NEWS

Thursday 23 November 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara aendelea na ziara yake wilayani Tarime Vijijini kuimarisha chama na kusikiliza kero za wananchiMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (kushoto mbele), akiongozwa na viongozi wa chama hicho alipowasili wilayani Tarime akitokea wilayani Serengeti, leo Novemba 23, 203. (Picha na Godfrey Marwa)
----------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Tarime
------------------------------


Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, leo Novemba 23, 2023 ameendelea na ziara yake ya kuimarisha chama, kukagua miradi ya maendeleo ya chama hicho tawala na kusikiliza kero za wananchi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Katika ziara hiyo, Chandi amefuatana na viongozi mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Marwa Daudi Ngicho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Simion Kiles Samwel na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara.

Kesho kiongozi huyo wa mkoa anatarajiwa kuendelea na ziara hiyo ya kimkakati katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages