NEWS

Monday 27 November 2023

Timu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu yatua mgodi wa Barrick North Mara kujionea fursa za ajira, uwezeshaji vijana na miradi ya kijamiiTimu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu mara baada ya kuwasili na kupokewa katika Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, leo Novemba 27, 2023.
-------------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara
Online News, Nyamongo
-----------------------------------


Timu ya Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu - wanaoshughulikia masuala ya kazi, vijana, ajira na watu wenye ulemavu, imewasili katika Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara, kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Timu hiyo ambayo inaongozwa na Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Yohana Madadi, imepokewa na Meneja Mahusiano wa Barrick North Mara, Francis Uhadi, leo Novemba 27, 2023.

Kwa mujibu wa Madadi, lengo la ziara hiyo ni kuona namna Kampuni ya Barrick na kampuni ya ubia ya Serikali ya Twiga zilivyotengeneza fursa za ajira, uwezeshaji vijana na jamii kwa ujumla katika eneo hilo.

Mara baada ya kuwasili, timu hiyo imepitishwa kwenye mada zinazohusiana na masuala ya ajira, uwezeshaji vijana na maendeleo ya jamii, utunzaji mazingira, ulinzi, mahusiano na tatizo la uvamizi unaofanywa makundi ya watu “intruders” mgodini hapo.


Wakurugenzi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu (kulia) wakiwa katika kikao cha kupitishwa kwenye mada za shughuli za mgodi huo. (Picha zote na Mara Online News)

“Tumekuja kuona uwekezaji wao katika maeneo haya, kufanya tathmini na kuangalia namna ya kushirikiana nao katika kutengeneza ajira na kuwezesha vijana,” amesema Mkurugenzi wa Ukuzaji Tija, Madadi.

Katika ziara hiyo, Madadi ameambatana na Wakurugenzi Joseph Nganga anayeshughulikia Huduma za Ajira, Dkt Mwiga Mbesi (Maendeleo ya Vijana), Amosi Nyandwi (Taarifa za Soko la Ajira) na Kissa Kilindu (Ukuzaji Ajira).

Kesho Jumanne, timu hiyo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu itatembelea na kujionea miradi mbalimbali ya kijamii, ukiwemo wa kilimo biashara kwa vijana uliowezeshwa na mgodi wa Barrick North Mara kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages