NEWS

Friday 3 November 2023

Waafrika wote sasa kuingia Rwanda bila visa



Rais Paul Kagame wa Rwara

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, ametangaza safari zisizohitaji visa kwa Waafrika wote, na hivyo Rwanda sasa imekuwa nchi ya nne barani Afrika kufanya hivyo.

“Pia tumeondoa vizuizi vya visa kwa raia wa kila nchi ya Afrika pamoja na mataifa mengine mengi. Mwafrika yeyote anaweza kupanda ndege hadi Rwanda wakati wowote anaotaka na hatalipa chochote kuingia nchini mwetu,” Rais Kagame alisema jana Alhamisi. 

Alisema hatua hiyo inalenga kufaidisha soko la utalii Afrika linalokua, likipigwa jeki na ukuaji wa uchumi wa kati barani humo. 

Rwanda imekuwa kwenye kampeni ya kukuza sekta yake ya utalii, ikishirikiana na vilabu vya soka kama Arsenal na Bayern Munich ili kuitangaza nchi hiyo kama kivutio cha watalii. 

Rwanda sasa inaungana na Ushelisheli, Gambia na Benin, nchi pekee za Kiafrika zinazotoa visa bila malipo kwa raia wote wa Afrika. 

Wiki hii, Rais wa Kenya, William Ruto alitangaza kuwa nchi hiyo itaondoa masharti ya visa kwa wageni wote wa Kiafrika ifikapo 2024. 

Hivi karibuni, nchi kadhaa za Afrika pia zimeingia makubaliano baina ya nchi mbili za usafiri wa bila visa. Nchi hizo ni Ghana na Afrika Kusini, na Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages