NEWS

Tuesday 21 November 2023

Waziri Mchengerwa awasimamisha kazi Wakurugenzi wa Halmashauri za Kibaha na IfakaraWaziri Mohamed Mchengerwa

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amewasimamisha kazi wakurugenzi wawili wa halmashauri kupisha uchunguzi dhidi yao.

Waliosimamishwa kuanzia leo Novemba 21, 2023 ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Ifakara mkoani Morogoro.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Jumanne na Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Serikalini katika Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah, imesema Waziri Mchengerwa amechukua hatua hiyo baada ya kupokea tuhuma za wakurugenzi hao kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Waziri Mchengerwa alimuagiza Katibu Mkuu TAMISEMU kutuma timu ya uchunguzi wa tuhuma hizo, ambapo ilibaini mapungufu ya wakurugenzi hao kushindwa kusimamia miradi ya maendeleo katika halmashauri zao.

Aidha, amewakumbusha wakurugenzi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kutekeleza majukumu yao kikamilifu, ikiwa ni pamoja na kusimamia miradi ya maendeleo, la sivyo hatasita kuwachukulia hatua stahiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages