NEWS

Friday, 13 March 2026

Rais Samia aweka msisitizo ulinzi wa Hifadhi ya Ngorongoro




Na Mwandishi Wetu
Ngorongoro
-------------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameendelea kusisitiza uhifadhi wa eneo la Ngorongoro kutokana na uwepo wa maliasili adhimu kwa faida ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Eneo hilo linasifika kwa utajiri wa bioanui, utalii, historia ya mwanzo wa maisha ya binadamu na utamaduni.

Rais alitoa msisitizo huo baada ya kupokea taarifa ya tume ya kutathmini mgogoro wa ardhi katika Hifadhi ya Ngorongoro na tathmini ya utekelezaji wa uhamisho wa hiari wa wananchi kutoka eneo hilo kwenda wilaya ya Handeni, mkoani Tanga.

"Serikali ina wajibu wa kulinda mfumo wa ikolojia unaounganisha Hifadhi ya Ngorongoro, maeneo ya Loliondo na Ziwa Natron," ilisema taarifa iliyotolewa na Ikulu jana.


Rais Samia akizungumza katika hafla hiyo

Rais Samia alisema nia ya uhamisho wa hiari ni kulinda mfumo huo wa ikolojia wenye manufaa kwa utalii na urithi wa dunia.

Alisema serikali itafanya marekebisho kuhusu kasoro zilizojitokeza kwenye awamu ya kwanza ya uhamisho wa hiari.

Kwa mujibu wa tume ya kutathmini mgororo wa ardhi eneo la Ngorongoro, ongezeko la watu, mifugo na makazi limezua shinikizo kubwa la matumizi ya ardhi, uharibifu wa mazingira na migongano ya binadamu na wanyamapori.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages