NEWS

Saturday 16 December 2023

Chandi achangisha milioni 602 kusaidia ujenzi wa jengo la mama na mtoto Nyamongo, wadau wakiwemo wakandarasi wazawa washirikiMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa akizungumza wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la mama na mtoto Nyamongo, juzi Ijumaa. Kushoto ni Mkurugenzi Mwanzilishi wa Shirika la HSF, Emmyliana Range aliyeandaa harambee hiyo.
-------------------------------------------------

Na Mwandishi wa Mara 
Online News, Nyamongo
------------------------------------

MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, ameongoza harambee ambayo imefanikisha kupatikana kwa shilingi milioni 602 na saruji mifuko 690, kwa ajili ya kusaidia mradi wa ujenzi wa jengo la ghorofa moja la mama na mtoto katika mji mdogo wa Nyamongo, wilayani Tarime.

Katika harambee hiyo ambayo ilifanyika juzi Ijumaa kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Ingwe, Chandi alichangia shilingi milioni tano taslimu.

Katika hotuba yake, Chandi ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema uboreshaji wa huduma za mama na mtoto ni moja ya maeneo yanayopewa kipaumbele na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

“Nitakuwa ninamleta kila waziri na viongozi wengine wanaofanya ziara mkoani Mara kuja kutembelea mradi huu ili kuhakikisha unakamilika,” alisema kiongozi huyo wa chama tawala.

Chandi alifuataa na viongozi mbalimbali akiwemeo Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Mara, Julius Masubo ambaye aliachnagia shilingi laki tano taslimu.


Mwenyekiti Chandi (kulia) akiwasili na kupokewa na Mkurugenzi Mwanzilishi wa HSF, Emmyliana (kushoto) kwa ajili ya kuongoza harambee hiyo.
-------------------------------------------------

Jumla ya fedha taslimu zilizoppatikana ni shilingi milioni 18.8, huku ahadi zikiwa shilini milioni 583 na saruji mifuko 690.

Wakurugenzi wa kampuni za wazawa zinaofanya kazi na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara walijitokeza kwa wingi kuchangia katika harambe hiyo iliyoandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Health and Safe Delivery Foundation (HSF).

Madiwani kutoka kata za Matongo na Kemambo walishiriki katika harambee hiyo na kuahidi kuendelea kuunga mkono juhudi za utekelezaji wa mradi huo.

Mkurugenzi Mwazilishi wa HSF, Emmyliana Range aliwashukuru wadau wote na viongozi walioshiriki katika harambee hiyo.

Emmyliana alisema ujenzi wa jengo hilo la mama na mtoto ni sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt Samia katika kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

“Unapookoa afya ya mama na mtoto umeokoa Taifa,” alisema Emmyliana ambaye ni kijana mzaliwa wa mji mdogo wa Nyamongo.

Ujenzi wa jengo hilo la mama na mtoto linatarajiwa kujengwa katika Kituo cha Afya Sungusungu (Nyangoto) kwa gharama ya takriban shilingi bilioni mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages