MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (mwenye skafu), amewasili wilayani Bunda leo Jumamosi kwa ziara ya kikazi, ambapo amepokewa na Mwenyekiti wa chama hicho wilayani humo, Ibraham Pius Mayaya.
Katika ziara hiyo, Chandi amefuatana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Mkoa wa Mara, Julius Masubo na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa.
Mwenyekiti Chandi (wa kwanza kushoto mbele) akiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mara katika ziara yake ya kikazi wilayani Bunda leo Jumamosi. (Picha zote na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment