NEWS

Sunday 10 December 2023

Dkt Mpango: Kazi aliyonituma Mungu sijaimaliza, akerwa na matumizi mabaya ya mitandaoMakamu wa Rais, Dkt Philip Isdor Mpango.
-------------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Dodoma
------------------------------------------


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Isdor Mpango, amewataka Watanzania kuwa na amani na kuondoa hofu iliyoenezwa na baadhi ya mitandao ya kijamii kwamba yeye ni mgonjwa, baada ya kutoonekana hadharani kwa muda wa zaidi ya mwezi.

“Mkae na amani… niko salama. Asanteni sana kwa kuniombea. Yamesemwa mengi. Na wengine bado wanasema mimi ni mzuka,” amesema Dkt Mpango wakati alipokaribishwa kuzungumza na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska, Kiwanja cha Ndege jijini Dodoma alipohudhuria ibada ya Jumapili leo.


Dkt Mpango (katikati) akibadilishana mawazo na Mapadre wa Kansa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska leo.

Dkt Mpango ameshangiliwa na waumini kwa nderemo na vifijo alipokariri Biblia kwa kutaja Zaburi ya 118 aya ya 17 inayosema: “Sitakufa bali nitaishi, nami nitayasimulia matendo ya Bwana.”

Makamu huyo wa Rais amesema baadhi ya watu wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kwa kuwaumiza watu wengine, jambo ambalo lazima likemewe kwa nguvu zote katika jamii inayojali utu na ustaarabu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages