NEWS

Monday 4 December 2023

Lori laanguka na kuteketea kwa moto Makutano mkoani Mara, watu wawili wadaiwa kupoteza maisha
Na Mwandishi wa
Mara Online News
---------------------------


Watu wawili wanasadikika kufariki dunia baada ya lori kuanguka ndani ya mto na kuteketea kwa moto leo asubuhi katika eneo la Makutano wilayani Butiama, Mara.

Taarifa za awali kutoka eneo la tukio zinasema lori hilo lilikuwa limebeba mafuta na kwamba chanzo cha ajali hiyo ni kufeli kwa breki zake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara hakupatikana haraka kwa ajili ya kuzungumzia ajali hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages