NEWS

Friday, 30 January 2026

Serikali yatoa bilioni 2/- kuwezesha watengenezaji wa maudhui ya mitandaoni kuimarisha kazi zao



Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-------------

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amesema wizara hiyo imepatiwa shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuwawezesha watengenezaji wa maudhui mbalimbali mitandaoni kuimarisha kazi zao na kuwaongezea kipato kupitia majukwaa ya kidijitali.

Akizungumza jijini Dodoma, Alhamisi Januari 29, 2026, Waziri Makonda alibainisha kuwa fedha hizo zimetolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa lengo la kuyawezesha makundi yote ya watengenezaji wa maudhui, ikiwemo katika sekta ya utalii, michezo, habari, jamii, muziki, filamu na sanaa nyinginezo.

Alisema uandikishaji wa walengwa unaanza rasmi Januari 30 hadi Februari 15, 2026, ambapo watengenezaji wa maudhui wanatakiwa kufika katika ofisi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa za Miji na Majiji kupitia vitengo vya habari, ili kuchukua na kujaza fomu za maombi, zikiainisha taarifa binafsi pamoja na shughuli wanazozifanya.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages