NEWS

Wednesday 20 December 2023

Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara katika ziara ya kikazi wilayani RoryaMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (wa kwanza kushoto mbele), akisalimiana na Mbunge wa Rorya, Jafari Chege, alipowasili wilayani humo kwa ziara ya kikazi leo. (Picha na Godfrey Marwa)
-------------------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News, Rorya
-----------------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, leo amewasili wilayani Rorya katika ziara yake ya kuimarisha chama, kukagua miradi ya chama, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua.

Kama kawaida, katika ziara hiyo Chandi ameambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya CCM Mkoa wa Mara, wakiwemo wabunge, wenyeviti na makatibu wa chama hicho tawala.Kwa ziara hiyo ya wilayani Rorya, kiongozi huyo amehitimisha awamu ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Mara. Tayari ameshafanya ziara katika wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime, Musoma Mjini, Musoma Vijijini na Butiama.


Mwenyekiti Chandi (wa tatu kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo jipya la CCM wilayani Rorya.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages