NEWS

Friday 8 December 2023

Sekondari ya Kambarage yapata msaada wa mabati kutoka Kampuni ya Utalii ya Nyamoyo AdventureMkurugenzi wa Kampuni ya Nyamoyo Adventure, Baraka Thobias (wa pili kulia) akikabidhi msaada wa mabati kwa uongozi wa Shule ya Sekondari Kambarage wilayani Serengeti jana Ijumaa.
-----------------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU, Serengeti
--------------------------------------------------

Kampuni ya Utalii ya Nyamoyo Adventure imeipatia Shule ya Sekondari Kambarage iliyopo wilayani Serengeti, Mara msaada wa mabati. 

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Baraka Thobias alikabidhi msaada huo kwa viongozi wa shule hiyo, akiwemo Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi na Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kanisani. 

“Leo tumefurhi kukabidhi msaada huu wa mabati kwa Shule ya Sekondari Kamabarage ili kuongeza nguvu ya ujenzi wa madarasa ambayo yatatumiwa na wanafunzi wa kidadyo cha tano na cha sita,” alisema Baraka ambaye alifutana na Afisa Mahusiano wa kampuni hiyo, Caren Werema. 

Alisema ni muhimu kwa kampuni za kitalii zilizowekeza katika wilaya ya Serengeti kusaidia maendeleo ya jamii ili wananchi waweze kuona matunda ya uhifadhi na utalii. 

Nyamoyo ni moja ya kamuni za kizalendo amabazo zipo katika mstari wa mabele kuhamasisha utalii katika mkoa wa Mara. 
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages