NEWS

Friday 8 December 2023

Waziri Aweso afanya mabadiliko madogo ya viongozi Wizara ya MajiWaziri wa Maji, Jumaa Aweso.
-----------------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU
--------------------------------------- 


Waziri wa Maji, Jumaa Aweso jana alifanya uteuzi wa viongozi watatu ndani ya wiazara hiyo. 

Alimteua Mhandisi Abbas Pyarali kuwa Mkurugenzi Msaidizi - Sehemu ya Usanifu na Usimamizi wa Miradi ya Maji Wizara ya Maji. 

Kabla ya uteuzi huo Mhandisi Pyarali alikuwa Mhandisi Mkuu katika Idara ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira, Wizara ya Maji. 

Mwingine ni Mhandisi Ndele Mengo aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi - Sehemu ya Uchimbaji wa Visima na Ujenzi wa Mabwawa. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mkurugenzi wa Ufundi RUWASA. 

Naye Mhandisi Mariam Majala aliteuliwa kuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Ufundi, RUWASA. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Simiyu. 

Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitendo cha Mawasiliano Wizara ya Maji, Florence Temba ilisema Waziri Aweso amefanya uteuzi huo kwa mamlaka aliyonayo kupitia Sheria Namba 5 ya Mwaka 2019 ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira. 
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages