NEWS

Friday 8 December 2023

Waziri Kairuki aiagiza TAWIRI kutafiti ufumbuzi wa migogoro ya binadamu na wanyamaporiWaziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki.
---------------------------------------------

NA MWANDISHI WETU, Arusha
------------------------------------------------

Serikali imeiagiza Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) kufanya tafiti zitakazosaidia kuondoa migogoro iliyopo kati ya binadamu na wanyamapori, kwa maendeleo ya sekta ya utalii. 

"Elekezeni nguvu zenu katika kushughulikia changamoto za migogoro ya binadamu na wanyamapori," Waziri wa Maliasili na Utalii, Angellah Kairuki aliagiza. 

Akifungua Kongamano la 14 la Kimataifa la Sayansi mjini Arusha juzi, Waziri Kairuki pia aliitaka TAWIRI kushughulikia upotevu wa makazi ya wanyamapori, kuziba kwa shoroba zao, mimea vamizi, magonjwa na kupungua kwa wanyama hao katika maeneo tengefu. 

Alisema uwepo wa maeneo mengi yanayoongoza kwa uhifadhi nchini kama vile Serengeti na Ngorongoro ni matokeo ya utafiti. 

TAWIRI pia imetakiwa kufanya utafiti wa kimkakati Kanda ya Kusini kuhusu ukuaji wa utalii kama ulivyo Kanda ya Kaskazini. 

Waziri Kairuki aliunga mkono pendekezo la kuanzishwa mfuko wa fedha wa kuboresha shughuli za utafiti za TAWIRI. 
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages