NEWS

Saturday 27 January 2024

Azania Bank Bunge Bonanza lafana jijini Dodoma, Spika Tulia akabidhi kombe
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
-----------------------------------------


WABUNGE na watumishi wa Bunge la Tanzania wameshiriki kikamilifu katika tamasha la Azania Bank Bunge Bonanza, ambalo limeweka rekodi ya kuwa moja ya matamasha ya bunge yaliyofana zaidi.Tamasha hilo ambalo liliandaliwa na Benki ya Azania, limefanyika leo Januari 27, 2024 katika viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma, likihusisha michezo 23 tofauti.


Mbunge wa Iramba Magharibi na Waziri wa Fedha, Dkt Mwigulu Nchemba ambaye ni shabiki wa Yanga, akiomba pasi wakati wa mchuano na Simba kwenye bonanza hilo.
----------------------------------------------
Kwa upande wa soka, wabunge na watumishi wa Bunge ambao ni mashabiki wa timu za Yanga na Simba wamechuana vikali, mbele ya mgeni rasmi, Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson.


Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt Tulia Ackson akikabidhi zawadi ya kombe kwa washindi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages