NEWS

Monday 15 January 2024

Balozi Dkt Nchimbi ateuliwa kuwa Katibu Mkuu CCMBalozi Dkt Emmanuel John Nchimbi
--------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imepokea na kuidhinisha pendekezo la Kamati Kuu (CC) ya Chama hicho - la kumteua Balozi Dkt Emmanuel John Nchimbi kuwa Katibu Mkuu wa CCM.

NEC hiyo imeridhia uteuzi huo wa Balozi Dkt Nchimbi kwenye kikao chake maalum, kilichoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, leo Januari 15, 2024 mjini Unguja, Zanzibar.

Balozi Dkt Nchimbi anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Daniel Chongolo aliyejiuzulu Novemba 2023.


Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Dkt Samia akisalimiana na Katibu Mkuu mpya wa Chama hicho tawala, Balozi Dkt Nchimbi, leo mara baada ya uteuzi wake mjini Unguja, Zanzibar,.
-----------------------------------------------

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages