NEWS

Tuesday 23 January 2024

Gachuma, Mtanda na Rhobi Samwelly wapitishwa na Halmashauri Kuu ya CCM Mara kuunda Kamati ya Usalama na Maadili, Mwenyekiti Chandi azindua tamasha Butiama




Na Mwandishi wa
Mara Online News
----------------------------


KIKAO Maalum cha Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, leo Januari 23, 2024 kimepitisha majina matatu ya wanachama wake watatu watakaounda Kamati ya Usalama na Maadili ya chama hicho mkoani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Mkoa wa Mara, Simon Rubugu imewataja wanachama hao kuwa ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Christopher Mwita Gachuma, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda na Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Taifa, Rhobi Pristiana Samwelly.


Mwenyekiti Chandi (aliyenyanyua mkono) akiongoza kikao hicho mjini Musoma leo.
---------------------------------------------------
Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa ambaye ametumia nafasi hiyo kuwashukuru wajumbe wa Halmashauri Kuu hiyo kwa kazi wanayofanya ya kukijenga chama hicho tawala.

Pia Mwenyekiti Chandi ameendelea kuwaomba wajumbe wa hao kuimarisha umoja katika kukijenga chama hicho tawala.
Aidha, Chandi amewajulisha wajumbe hao ujio wa ziara ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Omar Kinana mkoani Mara, itakayofanyika Januari 26, 2024.

Mara baada ya kikao hicho, Mwenyekiti Chandi ameelekea Butiama alikoalikwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa Tamasha la Michezo, Utamaduni na Ujasiriamali kuelekea kwenye Mkutano Mkuu wa Jimbo la Butiama, utakaofanyika Januari 26, 2024.


Mwenyekiti Chandi akikagua wachezaji wa mechi za uzinduzi wa tamasha hilo jimboni Butiama leo.
---------------------------------------------------
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Butiama, Jumanne Sagini, mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Kinana.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages