NEWS

Tuesday 2 January 2024

Kigogo CHADEMA ahojiwa na Jeshi la Polisi Mara kuhusu tuhuma za kupotea kwa watuJohn Heche

Na Mwandishi wa Mara Online News
------------------------------------------------


MJUMBE wa Kamati Kuu ya CHADEMA, John Heche, amehojiwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara kuhusiana na tuhuma za kupotea kwa watu katika mazingira ya kutatanisha.

“Tayari nimehojiwa kwenye ofisi ya RCO (Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa) Mara, na nimetoka hakuna shida,” Heche ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Tarime Vijijini ameambia Mara Online News kwa njia ya simu, muda mfupi baada ya kutoka kwenye mahojiano hayo mjini Musoma leo Januari 2, 2024.

Kada huyo wa CHADEMA amesema amehojiwa kuhusiana na taarifa ambazo amewahi kuandika kwenye mtandao wa kijamii akilituhumu Jeshi la Polisi kwa upotevu wa watu katika maeneo mbalimbali mkoani Mara.

“Nimehojiwa kwa zaidi ya saa moja hivi, na nimewapa taarifa ya watu waliopotea,” amesema Heche.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salum Morcase hakupatikana haraka ili kuzungumzia suala hilo, lakini awali alikaririwa na chombo cha habari cha mtandaoni akikiri jeshi hilo kumwita Heche kwa ajili ya mahojiano hayo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages