NEWS

Thursday, 11 January 2024

Kuji ateuliwa na Rais Samia kuwa Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Kihamia naye Mtendaji Mkuu mpya DART



Musa Kuji
----------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua Musa Kuji kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), baada ya kukaimu nafasi hiyo kwa miezi kadhaa.

Taarifa kwa umma iliyotolewa leo Januari 11, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus kutokea Zanzibar, inasema Rais Samia pia amemteua Dkt Athuman Kihamia kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART).

Kulingana na taarifa hiyo, Dkt Kihamia anachukua nafasi ya Dkt Edwin Mhede ambaye uteuzi wake umetenguliwa, na atapangiwa kazi nyingine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages