Na Mwandishi Wetu,
Dar es Salaam
--------------------------
Dar es Salaam
--------------------------
Ikorongo-Grumeti ni miongoni mwa mapori ya akiba yatakayonufaika na uwekezaji katika Maeneo Maalum ya Uwekezaji wa Wanyamapori (Special Wildlife Investment Concession Areas - SWICA), wenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 314 (sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 696).
Mikataba ya sita ya uwekezaji huo ilisainiwa jana jijini Dar es salaam mbele ya Waziri wa Maliasi na Utalii, Dkt Angellah Kairuki.
Mapori ya Akiba ya Ikorongo-Grumeti ambayo yapo mkoani Mara ni sehemu ya ikolojia ya Serengeti.
Maeneo mengine yatakayonufaika na uwekezaji huo ni Pori la Akiba la Mkungunero mkoani Dodoma na Mapori ya Akiba ya Maswa Kimali, Maswa Mbono na Maswa Kaskazini yaliyopo mkoani Simiyu.
Akizungumza na katika hafla ya utiajia saini mikataba hiyo, Waziri Kairuki alisema utekelezaji wa SWICA utaongeza utalii na mapato mapato kwenye maeneo ya uwekezaji huo, hali itakayochangia kwenye lengo la kuongeza idadi ya watalii nchini kutoka milioni 1.5 mwaka 2021/2022 hadi milioni tano mwaka 2025/2026.
Utiaji saini ukiendelea
“Uwekezaji huu utaingizia Serikali mapaoto yanayokadiriwa kufikia dola za Kimarekani milioni 314 katika kipindi cha miaka 20 ya uwekezaji sawa na dola milioni 16 (shilingi bilioni 40) kwa mwaka. Mafanikio haya yanatokana kwa kiasi kikubwa na utangazaji wa utalii kupitia “Filamu ya Tanzania -The Yoyal Tour,” alisisema Waziri Kairuki.
Waziri huyo mwenye dhamana ya Maliasili na Utalii alitaja manufaa mengine ya uwekezaji huo kuwa ni kuimarisha uhifadhi, utafiti na kuboresha maisha ya wananchi wanaoishi jirani na maeneo ya uwekezaji huo.
Kwa mujibu wa Waziri huyo, takriban dola za Kimarekani milioni 50 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 125 zitatumika kugharimia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya jamii katika kipindi cha miaka 20 ya uwekezaji huo.
Aidha, Waziri Kairuki alizipongeza kampuni za Grumeti Reserves Ltd, Bushman Safari Trackers Ltd, Mwiba Holdings Ltd na Magellan General Holdings Trading LLC kwa kufanikiwa kusaini mikataba ya uwekezaji mahiri.
Wadau wa uhifadhi wanasema uhifadhi wa Mapori ya Akiba ya Ikorongo-Grumeti hauna mbadala kutokana umuhimu wake katika uhifadhi endelevu wa ikolojia ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment