NEWS

Sunday 21 January 2024

Mwanafunzi wa kike wa kidato cha nne ajinyonga Tarime Vijijini




Na Mwandishi Wetu, Tarime
---------------------------------------


MWANAFUNZI wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari Gorong’a wilayani Tarime, amefariki dunia - ikidaiwa amejinyonga akiwa nyumbani kwao.

Tukio hilo lilitokea juzi Jumamosi, na marehemu ametambuliwa kwa jina la Vumilia Joseph Kihingo (17).

“Baada ya kutoonekana kwa muda tulifungua mlango wa nyumba anayolala binti yetu tukakuta ameishariki dunia,” Mwenyekiti wa Kitongoji cha Ngonje kilichopo kijiji cha Kenyamosabi katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), Matinde Chacha aliiambia Mara Online News jana Jumapili jioni.

Taarifa kutoka kwa ndugu wa binti huyo zinasema maafisa wa Jeshi la Polisi wakiwa wamefuatana na mtaalamu wa afya na walimu wa shule hiyo walifika eneo la tukio na kuthibisha kifo hicho.

“Walipompima walikuta amefariki, na atazikwa kesho [leo Jumatatu],” alisema mmoja wa wanafamilia.

Mara Online News inaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya kwa ajili ya kuzungumzia zaidi tukio hilo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages