NEWS

Thursday 25 January 2024

NECTA yatangaza matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne 2023, watahiniwa zaidi ya 100 wafutiwa kwa udanganyifu na matusi
KATIBU Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa Tanzania (NECTA), Dkt Said Mohamed (pichani), leo Alhamisi Januari 25, 2024, ametangaza matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kuhitimu Kidato cha Nne (CSEE), uliofanyika Novemba 13 hadi 30, 2023.

Dkt Mohamed alisema jumla ya watahiniwa 484,823 sawa na asilimia 87.65 ya wote waliofanya mtihani huo wamefauli.

Hata hivyo, alisema watahiniwa 101 wamefutiwa matokeo yote ya mtihani huo baada ya kubainika kufanya udanganyifu, huku watano wakifutiwa matokeo kutokana na kuandika matusi.

Aidha, NECTA imezuia kutoa matokeo ya watahiniwa 376 waliopata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani huo - baadhi kwa masomo yote na wengine kwa idadi kubwa ya masomo, alisema Dkt Mohamed.

Alifafanua kuwa NECTA imewapa watahiniwa hao fursa nyingine ya kufanya mtihani huo wa kidato cha nne.

Kutazama Matokeo  Bofya Hapa

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages