NEWS

Thursday 25 January 2024

Polisi Mara wamtia mbaroni mwanaume anayetuhumiwa kumuua mke wake kikatiliKamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salim Morcase (katikati) akisisitiza jambo.
------------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News
----------------------------


MKAZI wa kijiji cha Namhula wilayani Bunda, Muyengi Ruben (25), anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mara, akituhumiwa kumuua mke wake, Rosemary Malemi.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Mara, ACP Salim Morcase, Muyengi anadaiwa kutekeleza mauaji hayo Januari 20, 2024 saa 2:00 asubuhi, kijijini humo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Ruben alimfuata Rosemary shambani alikokuwa anapanda mpunga akiwa na mtoto wake, akamchoma na kitu chenye ncha kali juu ya titi la kushoto na nyuma ya bega la kulia - hali iliyomsababishia kuvuja damu nyingi hadi kupoteza maisha.

“Chanzo cha tukio hilo inadaiwa ni wivu wa mapenzi, baada ya mwanaume huyo kutaka kurudiana na mke wake na kukataliwa,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.

RPC Morcase alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi kuwa Jeshi la Polisi liko macho wakati wote, na halitasita kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages