NEWS

Friday 26 January 2024

Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar aachia ngaziSimai Mohamed Said
------------------------------

Na Mwandishi Wetu
------------------------------


WAZIRI wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar, Simai Mohamed Said amemuandikia Rais Dkt Hussein Ali Mwinyi barua ya kujiuzulu wadhifa huo.

Taarifa zinasema Waziri Simai aliandika barua hiyo na kujiuzulu kuanzia jana Januari 25, 2024 usiku.

“Nimefikia uamuzi huu ambao hapa kwetu si rahisi katika utamaduni wetu. Kutokana na imani yangu kwamba jukumu namba moja la wasaidizi wa Mheshimiwa Rais wakiwemo Mawaziri ni kumsaidia kutekeleza Ilani ya chama, na inapotokea mazingira yasiyo rafiki katika kutekeleza jukumu hilo muhimu kwa ustawi wa wananchi, ni vyema kutafuta jawabu kwa haraka ili kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo iweze kuendelea, na hata ikibidi kukaa pembeni.

“Mimi nimefikia uamuzi huo mgumu wa kukaa pembeni. Namshukuru Rais wa Zanzibar na Mwneyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Hussein Ali Mwinyi kwa kuniamini na kuniteua kuwatumikia Wazanzibar katika nafasi hii.

“Nitaendelea kuwa mtiifu kwa serikali pamoja na chama chetu - Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakati wote nitakuwa tayari kutoa ushauri wowote unaohitajika kwa serikali ili kuhakikisha ilani ya chama chetu inatekelezwa kikamilifu. Kidumu Chama Cha Mapinduzi, Kazi Iendelee,” alisema Simai katika taarifa yake ya kujiuzulu.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages