NEWS

Wednesday 24 January 2024

Rais Samia atua Indonesia kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatuRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno-Hatta, Tangerang kwa ajili ya ziara ya Kitaifa nchini Indonesia leo Januari 24, 2024.
--------------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
-------------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amewasili nchini Indonesia, ambapo atafanya ziara ya Kitaifa kuanzia leo Januari 24 – 26, 2024, kufuatia mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Indonesia, Joko Widodo.

Ziara hiyo inafuatia ziara ya Kitaifa ya Rais Widodo aliyoifanya nchini Tanzania, Agosti 2023.

Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba, ziara hiyo ya Rais Samia nchini Indonesia inalenga kukukuza na kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia na ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Indonesia, kupitia sekta mbalimbali za biashara na uwekezaji, kilimo, nishati, madini, mifugo, uvuvi, uchumi wa buluu, elimu, utalii na ulinzi.


Waziri January Makamba
------------------------------------
Matarajio ya ziara hiyo ni kuimarisha zaidi ushirikiano na uhusiano wa nchi hizo mbili. Aidha, wakati wa ziara hiyo inatarajiwa Hati za Makubaliano zitasainiwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages