NEWS

Tuesday 27 February 2024

Barrick North Mara Runners club yashiriki mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2024
Na Mwandishi Wetu, Kilimanjaro
--------------------------------------------


Barrick North Mara Runners Club, inayoundwa na wafanyakazi wa mgodi wa Barrick wa North Mara, ambayo imekuwa ikitamba katika mchezo wa mbio za marathon na kushiriki mbio nyingine mbalimbali, imeshiriki mbio za Kimataifa za Kilimanjaro 2024.

Mashindano ya mbio hizo yalifanyika mkoani Kilimanjaro hivi karibuni, ambapo baadhi ya washiriki kutoka Barrick North Mara Runners Club walimudu kukimbia mbio za masafa marefu.

Kampuni ya Barrick inayo sera madhubuti katika kusaidia wafanyakazi kwenye upande wa michezo kwa kuwa na miundombinu ya mazoezi kama gym, swimming pool na viwanja vya mpira wa miguu, kikapu na pete.

Pia inatoa vifaa na nyenzo mbalimbali za kufanyia mazoezi, pamoja na kugharimia wafanyakazi kushiriki mashindano yanayofanyika nje ya migodi yake ikiwemo nje ya nchi.

Kampuni pia kupitia kitengo cha Afya na Usalama huwa inaandaa mashindano ya ndani kwa kushindanisha idara mbalimbali, ikiwa ni njia mojawapo ya kuweka vizuri afya za mwili na akili za wafanyakazi wawapo kazini.

Kampuni ya Barrick pia imekuwa ikiandaa mashindano ya riadha yajulikanayo kama Bulyanhulu Healthy Lifestyle Marathon.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages