NEWS

Thursday, 3 July 2025

Dkt. Kamani atia nia ya ubunge tena Busega kupitia CCM



Dkt. Titus Mlengeya Kamani (kushoto) akirejesha fomu ya ubunge kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Busega, Steven Koyo, jana Julai 2, 2025.
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Busega

Aliyekuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi katika Serikali ya Awamu ya Nne na Mbunge wa Jimbo la Busega kati ya mwaka 2010 hadi 2015, Dkt. Titus Mlengeya Kamani, ameibuka tena kwenye ulingo wa siasa, akichukua na kurejesha fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea ubunge wa jimbo hilo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.

Dkt. Kamani alirejesha fomu hiyo jana Julai 2, 2025 na kuikabidhi kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Busega, Steven Koyo.

Dkt. Kamani ameguswa kurejea tena kwenye ulingo wa siasa ili kuendeleza harakati za kuwatumikia wananchi wa Busega kwa uadilifu, uzalendo na dira ya maendeleo endelevu.

Anaamini kuwa uzoefu wake wa kitaaluma na kiuongozi, ukiwemo uongozi wa wizara nyeti serikalini, unampa msingi imara wa kuendelea kushirikiana na wananchi katika kujenga Busega mpya iliyo na fursa kwa wote.

Hatua ya Dkt. Kamani kurejea katika kinyang’anyiro cha ubunge imechochea mjadala mpana wa kisiasa ndani ya wilaya hiyo, huku baadhi ya wachambuzi wakitafsiri kurejea kwake kama ishara ya kuimarika kwa mchuano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Kwa sasa, macho na masikio ya wapenzi wa siasa yanaelekezwa Busega, mkoani Simiyu kusubiri mwelekeo wa mchujo ndani wa CCM na hatimaye nani atapeperusha bendera ya chama hicho kuelekea Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages