NEWS

Tuesday 20 February 2024

Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini yawasili mgodi wa Barrick North MaraWajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakiwa ukumbini katika mgodi wa Barrick North Mara.
------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News, Tarime
-------------------------------------


KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imewasili katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara, unaoendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

Kamati hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, David Mathayo David, imepokewa mgodini hapo na uongozi wa Barrick leo Februari 20, 2024 asubuhi kwa ajili ya ziara ya kikazi.


Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda akizungumza.
------------------------------------
Mara baada ya kuwasili, Meneja wa Barrick nchini Tanzania, Dkt Melkiory Ngido amewasilisha kwa Kamati hiyo taarifa ya uwekezaji mkubwa wa Kampuni ya Barrick katika migodi yake ya North Mara na Bulyanhulu, pamoja na michango yake kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini Tanzania.


Dkt Ngido (katikati) akizungumza
-----------------------------------
Awali, Mkuu wa Mkoa, Mtanda, ameipongeza Kampuni ya Barrick kwa kuendeleza ushirikiano mzuri kwa Serikali.

Ziara ya Kamati hiyo itahusisha kutembelea ili kujionea shughuli mbalimbali za mgodi wa North Mara na miradi ya kijamii iliyotekelezwa kutokana na fedha zinazotolewa na mgodi huo kupitia mpango wake wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages