Na Mwandishi wa
Mara Online News, Tarime
-------------------------------------
Rais wa Poland Andrzej Duda amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili inayotegemewa kuibua fursa mbalimbali katika sekta kadhaa za uchumi wa nchini.
Sekta zinazotegemewa kufaidika na ziara ya Rais huyo ni kilimo, kodi, viwanda na biashara, utalii, elimu, usafiri,afya,tiba za mifugo na maji.
Fursa nyingine ni pamoja na maboresho katika sekta ya ulinzi na usalama, nishati, madini, ulinzi wa mitandao, utamaduni na uchumi wa bluu.
Akiwa nchini Rais huyo anatarajiwa pia kutembelea mradi wa matibabu ya dharula katika hospitali ya Agakhan Dar es Salaam ambapo atajionea utekelezaji wa mradi huo ambao serikali ya Poland imetoa ufadhili wa dola 1.136 milioni.
Mradi huo mbali na kuchangia maboresho katika huduma ya tiba kwa ujumla utasaidia pia kutoa elimu kwa wahudumu wa afya mkoani Dar es Salaam.
Baadae leo Rais Duda anatarajiwa kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Samia Suluhu Hassan Ikulu jijini Dar es Salaam na baadae kuzungumza na waandishi wa habari.
No comments:
Post a Comment