NEWS

Monday 11 March 2024

Chandi azindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Diwani Kata ya MshikamanoMwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi (kulia) akimnadi mgombea udiwani wa kata ya Mshikamano, Njofu Kamata kwa wananchi katani humo jana.
------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Musoma
----------------------------------------


MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Marwa Chandi jana Machi 11, 2024 alizindua kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Diwani wa Kata ya Mshikamano iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Musoma.

Katika uzinduzi huo, Chandi ambaye aliongozana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, alimtambulisha mgombea udiwani kata hiyo, Njofu Katama katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi.Mwenyekiti huyo wa CCM Mkoa wa Mara aliwaomba wananchi wa kata ya Mshikamano kumchangua Njofu ili ashirikiane na madiwani waliopo kuleta maendeleo kata ya kisekta katika kata hiyo.

Aliwahimiza wananchi wa kata hiyo kukipa ushindi chama hicho tawala katika uchaguzi huo, akisema ndicho chama chenye Ilani inayotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan.

Aidha, Chandi aliwadokeza wananchi hao kuwa kuna treni itapita Musoma na meli ya kisasa inayotoka Mwanza hadi Musoma mpaka Kisumu, Kenya, hivyo mizigo itashushwa katika mji huo na kuongeza mzunguko wa fedha kwa wananchi.Chandi alitumia nafasi hiyo pia kumkabidhi mgombea udiwani huyo wa kata ya Mshikamano kitabu cha Ilani ya CCM na kumwagiza kuwa baada ya uchaguzi huo utakaofanyika Machi 20, 024 aanze kutatua kero za wananchi katani humo, akianza na soko, pamoja na barabara ya lami.

Uchaguzi Mdogo wa Kata ya Mshikamano umekuja kuziba nafasi iliyoachwa wazi na diwani aliyekuwepo, Charles Mwita ambaye alifariki dunia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages