Diwani Lufunjo Mafuru Ndaro enzi ya uhai
-------------------------------------
Na Mwandishi Wetu, Bunda
---------------------------------------
DIWANI wa Kata ya Kisorya katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara, Lufunjo Mafuru Ndaro amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 67.
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Charles Manumbu na kijana wa Lufunjo, Mafuru Phinias Mafuru wamewambia waandishi wa habari kwamba diwani huyo amefariki dunia ghafla akiwa nyumbani kwake saa tisa usiku wa kuamkia leo Machi 15, 2024.
Kwa mujibu wa Mafuru, baba yake huyo amekuwa akihudhuria kwenye matibabu katika Hospitali ya Kamanga ya jijini Mwanza na kwamba daktari wake alisema alikuwa anaendelea vizuri.
Hata hivyo, Mafuru amesema familia inasubiri vipimo vya uchunguzi wa kitaalamu ili kujua chanzo cha kifo cha mzazi wake huyo, na kwamba mazishi yake yanatarajiwa kufanyika Jumatatu ijayo.
No comments:
Post a Comment