NEWS

Sunday 24 March 2024

Dkt Mkami afunguka jina lake kuhusishwa na ubunge Tarime Vijijini 2025Dkt Mwita Sospeter Mkami
-------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


KADA kijana wa chama tawala - CCM, Dkt Mwita Sospeter Mkami, ametoa ufafanuzi kuhusu suala la jina lake kuhusishwa na ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini kuelekea uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini mwaka 2025.

“Kwanza Katiba ya CCM inampa mwanachama wake mwenye sifa uhuru wa kuchagua na kugombea nafasi ya uongozi, hivyo wakati husika ukifika - kama wananchi wameamua, naamini tunaweza kujua nini cha kufanya, lakini kwa sasa tunatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi ya Mwaka 2020 - 2025,” amesema Dkt Mkami katika mahojiano na Mara Online News kwa njia ya simu leo Jumapili.

Dkt Mkami ambaye pia ni Mhadhiri wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania, amesema anachokifanya kwa sasa ni kushirikiana na wana-CCM wengine kumpa ushirikiano mbunge wa sasa wa Tarime Vijijini ili aendelee kutekeleza majukumu yake.

“Mbunge aliyepo madarakani ni Mwita Waitara, hivyo sisi wanachama wengine tunampa ushirikiano katika kutimiza majukumu yake ya kibunge,” alisema Dkt Mkami.

Hivi karibuni, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu naye alitoa ufafanuzi kuhusu tetezi zilizosambazwa kwamba mtangulizi wake katika nafasi hiyo, Zitto Kabwe atagombea urais mwaka 2025.

Semu alisema bado ni mapema kuzungumzia suala hilo, akisisitiza kuwa muda ukifika kila kitu kitakuwa wazi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages