Kanali Evans Alfred Mtambi.
---------------------------------------
Na Mwandishi Wetu
-----------------------------
-----------------------------
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Kanali Evans Alfred Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara.
Taarifa iliyotolewa leo Machi 31, 2024 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus inaeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Said Mohamed Mtanda amehamishiwa mkoani Mwanza kuchukua nafasi ya Amos Makalla.
Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Paul Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, akichukua nafasi ya John Mongella.
Kwa upande mwingine, Mkuu huyo wa nchi amemteua Deogratius Ndejembi kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu.
Naye Balozi Dkt Asha Rose Migiro ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Tume ya Mipango, miongoni mwa wengine kadhaa walioteuliwa kwa nafasi mbalimbali katika mabadiliko mapya yaliyofanywa na Rais Samia.
No comments:
Post a Comment