NEWS

Friday 29 March 2024

Katibu Mkuu CCM Dkt Nchimbi ahudhuria msiba nyumbani kwa MNEC GachumaKatibu Mkuu wa CCM, Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi (wa 5 kutoka kulia mbele) na viongozi mbalimbali waliokwenda kumpa pole na kumfariji MNEC Christopher Mwita Gachuma (wa 5 kutoka kushoto) nyumbani kwake mjini Tarime leo Ijumaa. (Picha na Mara Online News)
-------------------------------------------

Na Mara Online News, Tarime
-----------------------------------------


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt Emmanuel Nchimbi ameungana na viongozi mbalimbali wa chama, serikali na wananchi wa kawaida kuhudhuria msiba wa kifo cha mke wa Christopher Mwita Gachuma, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho tawala.

Balozi Dkt Nchimbi amewasili nyumbani kwa Gachuma mtaa wa Bomani mjini Tarime leo mchana, na kupata fursa ya kumpa pole na kumfariji MNEC huyo na familia yake.


Balozi Dkt Nchimbi (kushoto) akipokewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi nyumbani kwa MNEC Gachuma mjini Tarime leo Ijumaa, (Picha na Mara Online News)
-------------------------------------------

Mke wa Gachuma, Francisca, alifariki dunia ghafla akiwa nchini Kenya. Mwili wake umesafirishwa kwenda kijijini komaswa, Tarime kwa ajili ya mazisha yanayotarajiwa kufanyika kesho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages