Na Mwandishi Wetu
Miradi ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) katika sekta ya madini imezinduliwa wilayani Igunga mkoani Tabora.
Tume ya Madini mkoani Tabora ilishiriki katika uzinduzi huo uliofanywa jana na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, Sauda Mtondoo.
Miradi iliyozinduliwa ni ujenzi wa darasa moja na ofisi ya walimu katika Shule ya Msingi Mkwabi pamoja na ujenzi wa vizimba vya maji katika kijiji cha Nanga.
Malengo ya miradi hiyo ni kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujisomea na kuongeza upatikanaji wa huduma za maji safi na salama kwa jamii.
Miradi hiyo ya kijamii, kwa mujibu wa Tume ya Madini ya Mkoa wa Tabora, imetekelezwa na Kampuni ya Taur Tanzania Ltd kwa gharama ya shilingi milioni 50 katika mwaka wa fedha 2024/2025.
Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tabora, Nehemiah Mudala, alizitaka kampuni za uchimbaji madini kusaidia miradi ya maendeleo ya vijiji vinavyozunguka machimbo yao.
Naye Mkuu wa wa Wilaya, Sauda Mtondoo, alielezea umuhimu wa ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na jamii katika kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Aliipongeza Kampuni ya Taur Tanzania Ltd kwa mchango wake katika maendeleo kwa wananchi wa Igunga.



No comments:
Post a Comment