NEWS

Sunday 10 March 2024

Marekani yatuma meli ya kijeshi kujenga bandari Gaza




MELI ya kijeshi ya Marekani inasafiri kuelekea Mashariki ya Kati, ikiwa na vifaa vya kujenga gati ya muda kwenye pwani ya Gaza, jeshi limesema.

Meli hiyo ya msaada, inayojulikana kwa jina la Jenerali Frank S Besson JR, ilisafiri kutoka kambi ya kijeshi katika jimbo la Virginia jana Jumamosi.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais Joe Biden kusema Marekani itajenga bandari inayoelea ili kusaidia wakazi wa Gaza kupata msaada kwa njia ya bahari.

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa njaa katika ukanda wa Gaza ni "karibu isiyoepukika" na watoto wanakufa kwa njaa.

Uwasilishaji wa misaada kwa njia ya ardhi na anga umeonekana kuwa mgumu na hatari.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani lililazimika kusitisha usafirishaji wa barabara baada ya misafara yake kushambuliwa kwa risasi na uporaji.

Juzi Ijumaa kulikuwa na ripoti kuwa watu watano waliuliwa na kifurushi cha misaada kilianguka wakati parashuti yake iliposhindwa kufunguka vizuri.

Meli ya Marekani iliondoka "chini ya saa 36" baada ya Rais Biden kutoa tangazo lake, Kamanda Mkuu wa Marekani aliandika kwenye X.

"Inabeba vifaa vya kwanza vya kuanzisha bandari ya muda ya kupeleka vifaa muhimu vya kibinadamu" huko Gaza, taarifa hiyo iliongeza.

Pentagon imesema inaweza kuchukua hadi siku 60 kujenga bandari hiyo kwa usaidizi wa wanajeshi 1,000.
Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages