NEWS

Saturday 2 March 2024

Zanzibar: Rais Samia aongoza viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Ali Hassan MwinyiRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu wa Rais wa Namibia, Netumbo Nandi – Ndaitwah alipowasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kuongoza viongozi na wananchi kutoa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia Februari 29, 2024 katika Hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam alipokuwa akipata matibabu ya Saratani ya Mapafu, ambaye anazikwa kijijini kwake Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja leo Machi 2, 2024.


Askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwa na jeneza lenye mwili wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar leo Machi 2, 2024.


Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi enzi za uhaiViongozi Wastaafu mbalimbali wakiwa katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi leo Machi 2, 2o24.


Rais Samia akizungumza na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt Hussein Ali Mwinyi wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar leo Machi 2, 2024.


Wajane wa Hayati Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, Bibi Siti Mwinyi na Khadija Mwinyi wakiwasili katika Uwanja wa Michezo wa Amani mjini Zanzibar leo Machi 2, 2024.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages