NEWS

Sunday 3 March 2024

Mtoto mwanaharakati wa mazingira wa Kitanzania alivyohutubia mkutano wa kimataifaSharon Ringo akihutubia mkutano wa kimataifa jijini Nairobi, Kenya.
----------------------------------------

WIKI hii, mkutano maalum wa kimataifa unaohusu mazingira ulifanyika jijini Nairobi, Kenya na kuwaleta pamoja wanamazingira wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Miongoni mwao alikuwa ni binti mwenye umri wa miaka 13 kutoka Tanzania, Sharon Ringo ambaye hotuba yake iliyoangazia athari za mabadiliko ya tabianchi, iliyowagusa washiriki wengi wa mkutano huo.

Hotuba yake iliyotoa changamoto kwa serikali, wadau wa mazingira kuhakikisha kuwa watoto wanalindwa dhidi ya makali ya mabadiliko ya tabianchi.

“Na mimi ni mwanaharakati wa hali ya hewa. Niko hapa leo kwa sababu ulimwengu wetu unatishiwa. Wakati wangu ujao unatishiwa. Wakati ujao wa watoto wako unatishiwa. Watoto wanakufa. Sauti yangu leo ​​ni kwa mamilioni ya watoto na vijana duniani kote wanaoteseka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, uchafuzi wa mazingira na upotevu wa viumbe hai,” alisema.

Sharon kama watoto wengine duniani, amelivalia njuga suala la kuhamasisha ulimwengu kuwa watoto wana nafasi chanya pia kupambana na mabadiliko ya tabianchi.

Ana matumaini kuwa jitihada zake nchini Tanzania ni mojawapo wa juhudi ambazo ikiwa kila mtoto au mwanarika atawezeshwa kuhusika, basi makali ya mazingira yataanza kudidimia kadiri miaka inavyosonga mbele.

Tangu akiwa na miaka saba, Sharon alianza kudhihirisha dalili za uanaharakati katika umri huo mdogo.

“Nimeshiriki kupanda miti 49,000, kwa lengo la kupanda milioni 10. Sisi watoto lazima tupaze sauti zetu ili ulimwengu usikie kwamba tunahitaji mazingira ambayo ni ya kibichi, narudia TUNAHITAJI FUTURE YA KIJANI,” alisisitiza.

Binti anasema ni muhimu watoto kujumuishwa katika mipango inayohusu kipindi cha mazingira. 
BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages