NEWS

Saturday 16 March 2024

Rais Samia awafuta kazi vigogo wa Bodi ya Utalii, Hifadhi ya NgorongoroRais Dkt Samia Suluhu Hassan
-------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
------------------------------


RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Damasi Mfugale na kumteua Ephraim Mafuru kuchukua nafasi hiyo.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa juzi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, ilieleza kuwa Rais Samia pia ametengua uteuzi wa Kamishna wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya Eneo la Ngorongoro (NCAA), Richard Rwanyakaato Kiiza.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia pia amemteua Mhandisi Mwajuma Waziri kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, akichukua nafasi ya Prof Jamal Katundu ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Hali kadhalika, Rais Samia amemteua Ally Senga Gugu kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, na Kaspar Kaspar Mmuya kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages