NEWS

Friday 8 March 2024

Kishindo cha maadhimisho Siku ya Wanawake Duniani 2024 Barrick North Mara: Wafanyakazi wake wa kike wapeleka misaada kituo cha City of Hope, GM awafungulia jengo la ‘maternity’, 23 watunukiwa vyeti



Meneja Mkuu (GM) wa Mgodi wa Barrick North Mara, Apolinary Lyambiko (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wafanyakazi mgodini hapo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani jana Machi 8, 2024.
------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime
--------------------------------------


WAFANYAKAZI wanawake Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara jana Machi 8, 2024 waliadhimisha Siku ya Kimataifa ya Wanawake (International Women’s Day - IWD) kwa kupeleka msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea watoto cha City of Hope kilichopo kijiji cha Ntagacha wilayani Tarime.

Vitu walivyotoa msaada ni mahindi kilo 200, unga wa mahindi kilo 300, mchele kilo 400, maharage kilo 250, mafuta ya kula lita 120, sukari kilo 60, biskuti boksi 15, madaftari 2,000, kalamu boksi 50, penseli boksi 50, blanketi 140, ndala 105, mafuta ya kupaka katoni 20, taulo za kike na sabuni za kuogea na kufulia.

Baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Mgodi wa Barrick North Mara wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali katika kituo cha kulea Watoto cha City of Hope.
------------------------------------------
Meneja Mkuu wa kituo cha City of Hope, Cynthia Bhoke aliwashukuru wafanyakazi hao wa Barrick North Mara akisema: “Hakika mmevunja rekodi, hizi ni zawadi za kipekee, mmetoka na sisi mbali mnatusukuma kwenda mbele, tumefarijika sana Mungu awape baraka mnazostahili.”

Awali, GM Lyambiko alifungua jengo la ‘maternity’ kwa ajili ya wafanyakazi wanawake mgodini hapo, kisha akazungumza nao na kuwaeleza juhudi zinazofanywa na Barrick ili kuinua wanawake katika sekta ya madini.

GM Lyambiko akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa jengo la 'maternity' mgodini hapo.
----------------------------------------
Aidha, Kampuni ya Barrick iliwatunuku vyeti wafanyakazi wanawake 23 waliodumu kazini muda mrefu [miaka 10 hadi 20] mgodini hapo, huku Halima Mohamed Athuman akizawadiwa cheti maalum kama ishara ya kutambua mchango wake katika masuala ya usalama na miiko ya Kampuni ya Barrick Gold.
GM Lyambiko akikabidhi vyeti kwa wafanyakazi wanawake mgodini hapo.
-----------------------------------------
Kampuni ya Barrick Gold inaendesha mgodi huo tangu mwaka 2019 kwa ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.



Kilele cha Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu inasema “Wekeza kwa Wanawake Kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii.”


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages