NEWS

Saturday 13 April 2024

Makamu Mwenyekiti CCM Bara Kinana awasili Mara kuanza ziara ya kikazi, asimikwa kuwa Chifu wa Kabila la WaikomaMakamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana akipokewa kijijini Robanda, Serengeti mkoani Mara leo Aprili 13, 2024. Nyuma yake ni MNEC Christopher Mwita Gachuma aliyeongoza mapokezi hayo kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mkoa, Patrick Chandi.
--------------------------------------------------

Na Mwandishi wa
Mara Online News
-----------------------------


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara, Abdulrahman Kinana amewasili mkoani Mara leo Aprili 13, 2024 na kupata mapokezi makubwa yaliyoongozwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (MNEC), Christopher Mwita Gachuma kwa niaba ya Mwenyekiti wa Mkoa, Patrick Chandi.

Mara baada ya kupokewa katika kijiji cha Robanda wilayani Serengeti kwa ziara ya kuimarisha chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM mkoani Mara, Kinana amesimikwa kuwa Chifu wa kabila la Waikoma na kupewa jina la Marasi.Akizungumza kijijini hapo, Chiefu wa Kabila la Waikoma, Kenyatta Richard amesema hatua hiyo ya kumsimika Kinana ni ishara ya kutambua na kuthamini busara zake na utumishi wake ndani ya CCM katika kuwaongoza wanachama na kushughulikia changamoto za wananchi kwa ujumla.

Akizungumza baada ya kusimikuwa kuwa Chifu Marasi, Kinana amewashukuru wananchi wa Robanda kwa kumthamini na kumpa uchifu, na ameahidi kutendea haki wadhifa huo kwa kuendelea kutumia busara kuongoza ili kuwaletea Watanzania maendeleo.

Kwa upande wake, MNEC Gachuma amewashukuru na kuwapongeza wanachama wa CCM na wananchi wote waliojitokeza kwa wingi kumpokea Kinana kijijini Robanda.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages