NEWS

Wednesday 3 April 2024

Hapi Katibu Mkuu mpya Jumuiya ya Wazazi, Makalla amrithi Makonda Uenezi CCM TaifaAlly Salum Hapi
--------------------------

Na Mwandishi Wetu
-----------------------------


HALMASHAURI Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa, Ally Salum Hapi kuwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi ya chama hicho tawala.

Taarifa iliyotolewa na Idara ya Itikadi, Uenezi na Mafunzo ya CCM Taifa jioni hii, imeeleza kuwa NEC imefanya uteuzi huo kupitia kikao chake kilichofanyika jijini Dar es Salaam leo Aprili 3, 2024, chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan.

Pia kikao hicho kimemteua aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Amos Gabriel Makalla kuwa Katibu Mkuu wa NEC ya CCM, akichukua nafasi ya Paul Makonda aliyeteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella yeye ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, nafasi iliyokuwa inatumikiwa na Anamringi Macha ambaye ameteuliwa na Rais kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Naye Jokate Mwegelo ameteuliwa na kikao hicho kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), akichukua nafasi ya Fakii Lulandala ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages