NEWS

Thursday 4 April 2024

Rais Samia amwagiza Kanali Mtambi kusimamia vizuri rasilimali za mkoa wa Mara, ikiwemo Hifadhi ya SerengetiRais Dkt Samia Suluhu Hassan akimuapisha Kanali Evans Mtambi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara katika hafla iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo Aprili 4, 2024.
-----------------------------------------------

Na Mwandishi Wetu
----------------------------


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi kwenda kusimamia kikamilifu raslimali za mkoa huo, ukiwemo mto Mara na Hifadhi ya Taifa Serengeti.

“Nimekupeleka Mara kutokana na sifa nilizozisoma kwenye CV yako… weka urafiki mzuri wa kazi na Mkuu wa Mkoa wa Kagera msaidiane kuinua hiyo mikoa,” amemwagiza Kanali Mtambi.

Rais Samia ametoa maagizo hayo muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, katika hafla iliyofanyika Ikulu jijinki Dar es Salaam leo Aprili 4, 2024.

Amesema lengo kubwa la mabadliko ya viongozi aliyofanya ni kuimarisha ufanisi wa serikali katika kuwahudumia wananchi na kuwaletea maendeleo.


Rais Samia akizungumza baada ya kuwapisha viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
-----------------------------------------------

“Niwaombe kafanyeni kazi kwa kuwaunganisha watu, na nendeni katatueni migogoro, na msiende kutengeneza migogoro huko mnakokwenda,” Rais Samia amewasisitiza wateule wake hao.

Wateule wengine walioapishwa na Rais Samia katika hafla hiyo ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi, miongoni mwa wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages