NEWS

Monday 15 April 2024

Kinana ataka wavamizi mgodi wa North Mara wafikishwe kwenye vyombo vya sheria, Chandi amshukuru Rais Samia



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho Wilaya ya Tarime jana.
---------------------------------------------------

Na Godfrey Marwa, Tarime
-------------------------------------


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana amesema wavamizi wa Mgodi wa Dhahabu wa North Mara wanastahili kukamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria, si vinginevyo.

“Hakuna serikali inayoruhusu mwananchi [mhalifu] apigwe risasi mgodini, ni kinyume cha Katiba, ukimshika mtu mpeleke polisi. Kama kuna maeneo mgodi huyatumii vijana wapewe ili wasiingie ndani.

“Kamati ya usalama wa kitaifa inakuja hivi karibuni kutazama masuala ya kiusalama hapa, mtakaa nayo itawasikiliza malalamiko yenu kuhusu mgodi na Hifadhi ya Taifa Serengeti,” alisema Kinana wakati akihutubia mkutano wa wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Tarime jana.


Wajumbe mkutanoni
-------------------------------

Kinana alitumia nafasi hiyo pia kuwaonya wanachama wenye nia ya kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu kuacha kampeni za mapema.

Aidha, aliwataka wanachama kuwapa viongozi waliopo ushirikiano ili watimize majukumu yao ya kutekeleza Ilami ya chama hicho tawala.

Awali, akimkaribisha Kinana kuhutubia mkutano huo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuupatia mkoa huo fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi anazoleta Mara kwa ajili ya maendeleo, zawadi yetu kubwa kwake ni kura za kishindo,” alisema Chandi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages