NEWS

Thursday 18 April 2024

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Kenya afariki dunia katika ajali ya Chopa
NCHI ya Kenya imepata pigo baada ya Mkuu wake wa Majeshi ya Ulinzi (KDF), Francis Ogolla (pichani juu) miongoni mwa viongozi wengine kufariki dunia katika ajali mbaya ya helikopta iliyokuwa imewabeba.

Chopa hiyo imeanguka na kulipuka moto katika eneo la Kaber, muda mfupi baada ya kuondoka katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Cheptuel alasiri leo Alhamisi Aprili 18, 2024.

Taarifa kutoka NTV zinaonesha kuwa mamlaka imethibitisha vifo vya maofisa wengine kadhaa wa jeshi kutokana na ajali hiyo mbaya, huku watatu wakinusurika.

KDF Ogolla na viongozi wengine walikuwa katika ziara ya kutathmini hali ya usalama na kujadili uwezekano wa kufunguliwa kwa shule katika eneo la mpaka kati ya Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet.

Chanzo: TUKO.co.ke

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages