Na Mwandishi wa Mara
Online News, Tarime
---------------------------------
---------------------------------
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya, SACP Mark Njera amesema mwili wa mtu aliyepatikana akiwa amefariki dunia jana jioni katika eneo la kona ya Mrwambe kijijini Kewanja jirani na Mgodi wa North Mara unafanyiwa uchunguzi katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Kwa mujibu Jeshi la Polisi, mtu huyo anakadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 35 na 40.
“Tunasubiri uchunguzi wa daktari kubaini chanzo cha kifiko chake,” SACP Njera ameiambia Mara Online News ofisini kwake leo Aprili 8, 2024.
Kamanda Njera amesema hatua hiyo itawashirikisha ndugu wa marehemu endapo watapatikana na kwamba atatoa taarifa kamili ya tukio hilo baada ya matokeo ya uchunguzi.
Mgodi wa Dhahau wa North Mara unaendeshwa na kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia kampuni ya Twiga Minerals.
No comments:
Post a Comment