NEWS

Monday 29 April 2024

RC Makonda aanza na watuhumiwa wizi wa fedha za TASAF Arusha



Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda.

NA MWANDISHI WETU, Arusha
--------------------------------------------


MKUU wa Mkoa (RC) wa Arusha, Paul Makonda ameagiza kupandishwa mahakamani kwa watendaji wa mkoani humo waliohusika na upotevu na wizi wa shilingi milioni 428 zilizotengwa na serikali kwa ajili ya mpango wa kunusuru kaya maskini kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF).

RC Makonda alitoa agizo hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa wiki iliyopita, baada ya kukamilika kwa uchunguzi uliokuwa ukifanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Aidha, aliiagiza TAKUKURU Mkoa wa Arusha kufanya uchunguzi ili kujiridhisha na thamani ya fedha kwenye miradi ya TASAF inayotekelezwa katika mkoa huo.

Sambamba na hilo, alitangaza kuanza kwa uchunguzi maalum kuhusu matumizi ya fedha zinazotolewa na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Arusha, na kuahidi kuchukuliwa kwa hatua za kisheria dhidi ya watakaobainika kuzihujumu.

RC Makonda alitumia nafasi hiyo pia kutoa onyo kwa watendaji wabadhirifu na wezi wa fedha za serikali akisema hatafumbia macho mtu yeyote anayekwenda kinyume na maadili ya utumishi wa umma.
Chanzo: Gazeti la SAUTI YA MARA
#Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages