NEWS

Monday 29 April 2024

Simba azua hofu kwa wanakijiji jirani na Hifadhi ya SerengetiSimba (picha ya maktaba)

Na Mwandishi Wetu
Mara Online News
----------------------------


MAMLAKA za serikali zimeombwa kumsaka na kumwondoa simba anayedaiwa kuvamia kijiji cha Mrito na kuzua hofu kubwa kwa wananchi.

Kijiji cha Mrito kipo umbali wa kilomita chache kutoka lango la Lamai la Hifadhi ya Taifa Serengeti, mashariki mwa wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Maulid Hassan Surumbu alielezwa kuwa simba huyo amekuwa akionekana kwenye baadhi ya vichaka, na tayari ameshaua mifugo kadhaa ya wananchi kijijini hapo.

Wakazi wa kijiji hicho waliwasilisha kero hiyo kwa kiongozi huyo wakati alipokuwa kwenye ziara ya kufuatilia athari za mafuriko katika bonde la mto Mara wiki iliyopita.

Kanali Surumbu aliahidi kuwasiliana na maofisa wa wanyamapori kwa ajili ya kumsaka na kumrejesha hifadhini, au kumuua simba huyo kabla hajasababisha madhara zaidi kwa wananchi kijijini Mrito.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages