NEWS

Thursday 25 April 2024

Tarime Vijijini: Barabara yafungwa kupisha matengenezo daraja la mto Tigithe
Na Mara Online News
------------------------------


BARABARA ya Nyansangero-Kona Nne katika kata ya Nyamwaga wilayani Tarime, Mara imefungwa kwa muda kupisha matengenezo ya daraja la mto Tigithe.

“Daraja la mto Tigithe limeharibika, hivyo mkandarasai ambaye amepewa kazi na TARURA ameifunga ili aendelee na kazi ya utengenezaji wa daraja,” Diwani wa Kata ya Nyamwaga, Mwita Marwa ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu mapema leo.

Hata hivyo, Mwita hajajua matengenezo ya daraja hilo yatachukua muda gani ili kurejesha usafiri kwa mamia ya wananchi wanaotumia barabara hiyo iliyopo jirani na mgodi wa Dhahabu wa North Mara.

“Sijui muda ambao watatumia lakini tunataka kazi iishe kwa haraka na sasa hivi tunaomba wananchi watumie barabara ya Nyamwaga-Kona Nne,” amesema diwani huyo kutoka chama tawala - CCM.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages