NEWS

Thursday 16 May 2024

Baadhi ya Vilabu ligi kuu Uingereza vinataka mfumo wa VAR uondolewe



Mfumo wa Teknolojia ya VAR unaomsaidia muamuzi wa mechi za soka katika kufanya maamuzi uwanjani
-------------------------------------------


Ligi Kuu ya Uingereza inaweza hivi karibuni kuondoa VAR kwani vilabu vimepanga kupiga kura mwezi ujao ili kuamua hilo.

VAR ni mfumo wa uamuzi unaotumia teknolojia ambao unalenga kusaidia waamuzi uwanjani kufanya maamuzi sahihi wakati muhimu katika mechi za soka.

Katika miaka michache iliyopita, Msaidizi wa Mwamuzi wa Video au VAR imekuwa sehemu muhimu ya mechi za soka.

Mashindano makubwa zaidi ya soka duniani, ikiwa ni pamoja na Premier League, Bundesliga, Euro na Kombe la Dunia la FIFA yote yameanza kutumia VAR.

Wolves Moja ya vilabu vinavyoshiriki ligu kuu nchini Uingereza wameanza mchakato wa kufuta mfumo huo, na mpango wao utakuwa katika ajenda tarehe 6 Juni.Hata hivo mabadiliko yoyote ya sheria yanahitaji angalau wajumbe (vilabu) 14 kati ya 20 ili kupitishwa na kuthibitishwa rasmi.

Maoni ya wadau kuhusu iwapo teknolojia ya VAR iondolewe au iendelee kutumika:

Watumiaji wa mitandao ya kijamii pia hawakubaki kimya kuhusu suala hilo na kutoa maoni yao.

Min Faithman kwenye Facebook aliandika:

"Ndiyo waondoe. Iliundwa kufaidi wachache kwa hasara ya wengi na watu wanaoendesha VAR huko Uingereza ni wafisadi sana. Ligi ya Mabingwa Ulaya inapaswa kufanya hivyo pia"

Deng Bol Matong pia alitoa maoni Facebook akisema,

"Ronaldo alifunga karibu mabao manne na yote kukataliwa na VAR kwa hivyo VAR ni muhimu lakini wanahitaji kuboresha zaidi"

Kwa upande mwingine, Kocha wa zamani wa Chelsea, Real Madrid na hivi karibuni AS Roma ya Italia, Jose Mourinho, alipoulizwa maoni yake juu ya VAR, alisema;

"Ni wezi tu wanaoweza kulalamika juu ya uanzishwaji wa kamera za usalama", kauli inayoonyesha wazi kuwa anapinga mpango wa baadhi ya Vilabu Ulaya kutaka teknolojia ya VAR iondolewe.
 
Chanzo:Fabrizio Romano













No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages